Timu ya Super Eagles ya Nigeria imeondolewa kutoka kwenye mashindano ya kuwania kombe la taifa bingwa la Afrika CHAN Kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi za nyumbani.
Nigeria Ambao ni miongoni mwa Vigogo wa soka ya Afrika hawakuweza kufurukuta baada ya bao la Ibrahima Sankhon lililoiweka Guinea mbele kunako dakika 45 ya kipindi cha kwanza.
Timu ya Super Eagles ilianza mechi hiyo ikihitaji ushindi ama hata sare ya aina yeyote kusonga mbele lakini Guinea ilikuwa na mipango tofauti. Na baada ya nipe nikupe na mechi iliyokuwa na kasi , Guinea walifunga bao na kisha wakarejea nyuma kulinda lango lao.
Guinea hata hivyo walimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya wapinzani wao wakuu Tunisia. Tunisia walithibitisha wao ni moto wa kuotewa mbali baada ya kuiadhibu vikali Niger mabao 5-0 .
Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Nyamirambo na Kufuatia ushindi huo Tunisia inaongoza kundi hilo la Cha ikifwatwa kwa karibu na Guinea.
Washindi hao wawili sasa watasubiri hadi leo kujua nani watakayechuana nao kati ya Uganda na Zimbabwe. Awali Cameroon ilijikatia tikiti ya kusonga mbele kwa kuinyuka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo 3-1.
Vilevile Ethiopia iliambulia kichapo cha 1-2 dhidi ya Angola. Mechi inayotazamiwa na wengi ni ile kati ya DRC dhidi ya Amavubi ya Rwanda. Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa taifa wa Amaghoro.