Manchester United wamekanusha habari kwamba walikutana na kuzungumza na meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano wake kuwa meneja wao.
Tovuti ya France Football ilikuwa imesema mkutano huo ulifanyika mjini Paris lakini United wamesema habari hizo si za kweli. Meneja wa sasa wa United Louis van Gaal amekabiliwa na shinikizo baada ya klabu hiyo kutofanya vyema ligini Uingereza na Ulaya.
Guardiola, 45, anataondoka Bayern Munich majira yajayo ya joto na amesema amepokea maombi kutoka kwa klabu kadha za Uingereza. Manchester City wamo kwenye nafasi nzuri ya kumchukua, lakini Chelsea na United wamedaiwa kumtafuta pia.
Awali ilisemekana Pep Guardiola amesema kwamba atahama klabu ya Bayern Munich mwisho wa msimu na kwenda kusimamia timu Uingereza.
Meneja huyo wa zamani wa Barcelona amesema hataongeza mkataba wake Ujerumani, utakapomalizika mwisho wa msimu huu