Yanga Sc Sasa Hii Sifa, Yarudi Kileleni Ikipiga 5-0 Taifa

Yanga-2

Klabu ya Yanga Imefanikiwa kurejea Keleleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara mara baada ya ajana kuiibuka na ushindi wa bao 5-0 dhii ya wanalizombe timu ya majimaji.

Yanga walianza kupata bao lao la kwanza kupitia kwa Thabani Kamusoko ambaye alipachika bao hilo dakika ya nne kipindi cha kwanza kwa kutumia makosa yaliyofanywa na golikipa wa Majimaji FC David Burhani aliyesogea mbele na kuliacha lango lake wazi.

Bao hilo lilidumu hadi dakika zote za kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Majimaji.

Donald Ngoma alipachika bao la pili dakika ya 50 kipindi cha pili na kuiweka Yanga mbele kwa bao mbili mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Yanga-1

Gharika ya magoli ilianza baada ya Majimaji kuruhusu bao la pili, kwani Amis Tambwe ndiyo ukawa muda wake wa kutafuta (hat-trick) nyingne kwenye ligi ya msimu huu. Dakika ya 60 Tambwe alizama wavuni kuiandikia timu yake bao la tatu huku likiwa ni bao lake la kwanza kwenye mchezo huo.

Tambwe alipachika bao jingine la pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Deus Kaseke ambaye alimuwekea krosi Tambwe naye akaitupia kwenye nyavu. Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Burundi alikamilisha hat-trick yake dakika ya 84 baada kupiga goli safi kufuatia beki wa Majimaji kujiangusha kwenye eneo lake la hatari na kutoa mwanya kwa Tambwe kufunga goli kwa urahisi.

Mchezo wa jana ulikuwa ni wa pili kwa Kally Ongala tangu akichukue kikosi cha Majimaji akiwa kama kocha mkuu wa timu hiyo na kujikuta akiambulia kichapo cha nguvu kutoka kwa Yanga.

Yanga-3

Matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa kwenye viwanja tofauti

Januari 21, 2016
Yanga SC 5-0 Majimaji
Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar
African Sports 0-0 Mtibwa Sugar

Januari 20, 2016
JKT Ruvu 0-2 Simba SC
Mgambo JKT 1-2 Azam FC
Stand United 2-1 Toto Africans
Ndanda FC 3-1 Mbeya City
Prisons 2-1 Coastal Union

Wafungaji Ligi Kuu Tanzania Bara
1: Tambwe Amissi 13
2: Hamisi Kiiza 10
3: Donald Dombo Ngoma 9
4: Elias Maguri 9
5: Kipre Herman Tchetche 8