MKURUGEZI Mtendaji wa Haki ya Elimu, John Kalage amesema ubora wa Elimu umekuwa ni changamoto ya muda mrefu na sasa ni muda muafaka kwa Serikali kuandaa mikakati itakayo wezesha elimu katika ngazi zote.Akizungumza Dar es Salaam leo
wakati wa
uzinduzi wa Waraka wa Hakielimu juu ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka
2014 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam Kalage, alisema njia pekee za kufanikisha suala hilo ni kuwa na shule bora za umma ambazo zinahudumia wanafuzi wengi kuwa na walimu bora na wenye hamasa ya kufundisha kuwa na mifumo ya kufuatilia na kutathimini kiwango cha elimu katika ngazi zote na mifumo bora ya usimamizi wa shule.“Napenda kuipongeza Serikali kwa juhudi za kuhakikisha sera ya elimu na mafuzo ya 2014 inapatikana, hii ni baada ya kuwepo kilio cha mda mrefu kwa umma na wadau wa elimu kudai kufanyiwa marekebisho kwa sera za elimu za zamani ambazo zilishapitishwa na wakati ni hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto mpya za elimu,” alisema.
Mkurugezi huyo alitolea ufafanuzi suala la kuboresha elimu alisema malengo ya sera yanatarajia kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa nchini inakuwa bora na ya viwango vya ushindi.
Alisema katika uchambuzi wameonesha tafiti nyingi zinakubali kuwa elimu inayotolewa iwe yenye ubora kwani nimuhimu taifa lijitahidi kuboresha mazingira ya ufundishaji na kuwekeza katika ubora wa walimu ambao ndio msingi wa elimu yenyewe.
Kalage alisema ni muhimu Tanzania ifanye tathmini na kuweka bayana msimamo wake kuhusu lugha itakayo tumika kuelimisha jamii na kizazi kijacho.
“Hakielimu inaona kuwa njia pekee ya kutatua suala hili ni kuchagua lugha ambayo itaendana na uwekezaji ili kuwe natija katika ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi ili wapate maarifa na ujuzi unaostahili na kuweza kushindana katika masoko ya ajira kimataifa,” alisema Kalage.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugezi wa Sera na Mipango Chonya Caristus, alisema Serikali imekamilisha mikakati yote ya sera hiyo na wanachosubiri ni maboresho ya mwisho.