Timu ya DRC imeanza kampeni yake ya kutaka kushinda kombe la Ubingwa wa Afrika kwa mara ya pili vyema baada ya kuicharaza Ethiopia 3-0 katika mechi ya ufunguzi wa kundi B.
DR Congo ilioshinda michuano ya CHAN mwaka 2009,ilitawala mechi hiyo iliochezwa katika mji wa Butare nchini Rwanda,huku Guy Lisadisu akiwaweka kifua mbele kunako dakika ya 44.
Baada ya mapumziko ,Chui hao wa DRC waliendeleza juhudi zao na kunako dakika ya 46 Heritier Luvumbu alifunga kupitia kichwa huku Mechack Elia akiongeza bao la tatu dakika tisa baadaye.
Hatua hiyo ina maanisha kwamba timu ya Walia kutoka Ethiopia wanatafuta ushindi wao wa kwanza katika historia ya michuano hiyo.nayo Angola iliambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Cameroon
Michezo ya leo tarehe 18/01/2016
Tunisia vs Guinea – 16:00
Nigeria vs Niger – 19:00