Basi la Airbus Lamkanyaga Fundi Wake na Kumuua

Maofisa wa Polisi Usalama Barabarani waking'oa namba za usajili wa basi hilo baada ya kubaini linatatizo na kuliamuru likarekebishwe kabla ya kuanza safari muda mfupi kabla ya ajali kutokea.

Maofisa wa Polisi Usalama Barabarani waking’oa namba za usajili wa basi hilo baada ya kubaini linatatizo na kuliamuru likarekebishwe kabla ya kuanza safari muda mfupi kabla ya ajali kutokea.

BASI la Kampuni ya Airbus linalofanya safari zake kwenda Tanga kutokea Dar es Salaam limemkanyaga fundi wake na kumuua papo hapo. Ajali hiyo imetokea wakati fundi huyo pamoja na wenzake wakilitengeneza basi hilo katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo ambapo lilizuiliwa kusafirisha abiria hadi lifanyiwe matengenezo ambayo wakaguzi wa polisi waliyabaini kabla ya kuanza safari.
Taarifa za mashuhuda zinasema basi hilo baada ya kugundulika kuwa inatatizo iliamuriwa kushusha abiria na kurejea kwenye matengenezo kabla ya safari na ndipo ilipotokea ajali ya kumuua fundi wake.

“…Hii basi lilikaguliwa na askari na kugundulika na kasoro. Baada ya kupewa maelekezo ya kuzunguka gereji. Ilikata fock ya gear box. Gear zikawa hazifanyi kazi. Mafundi wao walianza matengenezo na kufungua top cover ya gear box wakapaga gear na mafundi wawili wakatoka na kumwamuru dereva aendeshe gari. Dereva kawasha gari ikiwa kwenye gear akaondoka kumbe chini kabaki fundi mmoja ambae ndio marehemu alikuwa anashusha jeki tairi ya nyuma na kumpanda mwili wake wote na kupasua kichwa,” kilisema chazo kimoja cha habari kutoka eneo la tukio.