Mbunge Segerea Azinduwa Kampeni Elimu Bora

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (katikati) akizungumza na wanahabari kuelezea namna kampeni ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora katika Jimbo lake itakavyofanya kazi.

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (katikati) akizungumza na wanahabari kuelezea namna kampeni ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora katika Jimbo lake itakavyofanya kazi.


MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA ,ni kampeni isiyo na malengo ya kumnufaisha mtu binafsi bali inalenga kuisaidia jamii ndani ya jimbo la Segerea katika upatikanaji wa elimu bora kupitia maboresho ya miundombinu ya shule kama madarasa, vyoo, mifumo ya maji safi na salama, madawati na kadhalika.
Ndugu zangu ninyi wote ni mashahidi kuwa zipo changamoto nyingi katika sekta ya elimu ndani ya nchi yetu zinazohusiana moja kwa moja na masuala niliyoyataja hapo juu.Huku tukilenga kupata;
•madawati 15,000,
•matundu ya vyoo vya kisasa 1335,
•visima vya maji 12, na
•vyumba maalum vya watoto wa kike 38.
Kimsingi kampeni hii ni muendelezo wa kampeni iliyowahi kufanyika katika kata ya KIPAWA [ndani ya jimbo la Segerea] kwa kusimamiwa na mfuko wangu wa elimu uitwao BONNAH EDUCATION TRUST FUND mnamo mwaka 2011,kipindi nilipokuwa diwani wa kata hiyo.Kwakuzingatia mafanikio na matokeo chanya ya kampeni hii katika ngazi ya kata;
Kwa moyo wa dhati kabisa, kwakuwa nimechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Segerea ,nimedhamiria kupeleka mafanikio ya kampeni hii kwa kushirikiana na mfuko wangu wa BONNAH EDUCATION TRUST FUND katika ngazi ya jimbo ili basi kila mwananchi ndani ya jimbo la Segerea anufaike na kampeni hii.
Ili kufanikisha kampeni hii, tutawashirikisha wadau mbalimbali wa elimu waliopo ndani na nje ya jimbo la Segerea kama vile Serikali, Makampuni, Mashirika na watu binafsi.

Kampeni ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA tunatarajia kuifanya kwa awamu mbili ambazo ni;
¡. Matembezi ya hiyari (Charity walk) na
¡¡. Chakula cha jioni (Gala dinner).

MATEMBEZI YA HIYARI.
Matembezi haya yatafanyika ndani ya jimbo kwa kushirikisha wananchi ,na wadau wote wa elimu tukiwa na lengo moja tu la kukusanya fedha za kuboresha miundombinu ya elimu katika jimbo letu la Segerea kwa shule za msingi katika kata zote kumi na tatu[13] za jimbo la Segerea.
Matembezi haya yanatarajiwa kufanyika tarehe 25/02/2016, kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 alasiri.
CHAKULA CHA JIONI
Awamu hii ya pili na ya mwisho ya kampeni yetu inatarajiwa kufanyika tarehe 03/06/2016 kuanzia saa 2 usiku na kuendelea.
Katika awamu hii tunatarajia kuwa na chakula cha jioni cha pamoja ambapo wageni kutoka maeneo mbali mbali na nje ya nchi watashiriki nasi katika kuchangia na kuhamasisha upatikanaji wa fedha na mahitaji yote muhimu kuelekea ufanikishaji wa kampeni yetu.
Tunawashukuru ninyi waandishi wa habari na wageni wote waalikwa kwa kushiriki nasi katika uzinduzi huu wa kampeni hii ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA jimbo la Segerea.
Hivyo natangaza rasmi kuwa kampeni hii imezinduliwa rasmi leo tarehe 17/01/2016.
Ahsanteni sana
Mawasiliano
Mh.Bonnah Kaluwa ; 0758 324 552
Bi. Jackline; 0713 711 632
Bw.Shamsudin; 0713 754 869