Dirisha Dogo La Ushajili Linavyowaumiza Vichwa Wanasoka

Bayer Leverkusen v Villarreal - UEFA Europa League

Mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani Stefan Kiessling aliyekuwa mbioni kujiunga na Hanover katika kipindi hiki cha uhamisho wa dirisha dogo, ameamua kubaki katika klabu yake ya Bayer Leverkusen.

Kiessling ameliambia gazeti la Bild kuwa nusra ahame baada ya kukasirishwa na sehemu ya kwanza ya msimu ambao mchezaji Javier “Chicharito” Hernandez aling’ara katika safu ya mashambulizi baada ya kusajiliwa akitokea Real Madridi.

845f14a6229b13a50abd16399e222db9

Naye Mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Ilkay Gündogan hajausaini mkataba wa muda mrefu na Borussia Dortmund wakati kiungo huyo akitafakari ikiwa ataongeza mkataba wake utakaomalizika mwakani au ahamie katika klabu mpya

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa katika klabu ya Dortmund tangu 2011, alidokeza mwaka jana kuwa angeondoka huku vilabu kadhaa nchini Italia na Uingereza vikimtaka, kabla ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili mwezi Julai.

Gündogan ameliambia gazeti la Bild kuwa hajafanya uamuzi wowote na lazima atathmini kila kitu kwa sababu urefu wa taaluma ya mtu una ukomo. Ameongeza kuwa kila kitu kingali wazi, na kuwa mkataba wake ujao utakuwa mrefu na sio wa mwaka mmoja tu.