Winga wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez anatarajia kurejea dimbani mwishoni mwa wiki ambapo timu hiyo itakapoumana na Sunderland katika Kombe la FA.
Mchezaji huyo raia wa Chile alikuwa nje ya uwanja tangu Mwezi wa kumi na Moja mwaka uliopita baada ya kupata majeraha wakati Arsenal walipokuwa wakipambana na Norwich City.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitarajia kurudi kabla ya Christmas lakini meneja wa klabu hiyo Mzee Wenger akampa muda zaidi wa kupona jeraha lake, hivyo kurudi kwake atakuwa ameongeza nguvu katika kikosi hicho watakapo pambana na Liverpool katika mchezo wa ligi wiki ijayo na Chelsea
Wenger amesema kurejea kwa Sanchez kutamsaidi Ozil na Nacho Monreal kupata mapumziko pia.