Hans Poppe Aunga Mkono Simba Kupigwa Bei

SONY DSC
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba anaunga mkono klabu kuingia katika mfumo wa kuuza hisa.
Poppe amesema pia anaafiki Mohammed ‘Mo’ Dewji kununua asilimia kubwa ya hisa za klabu.

amesema amelazimika kuelezea msimamo wake baada ya kuibuka kwa vikundi vya watu vikisambaza habari za upotoshaji kwamba yeye anampinga Mo kununua hisa nyingi za klabu hapo msimbazi

“Kusema eti mimi nilikaa kikao na Wazee (wa Simba) kupinga Mo kununua hisa nyingi za klabu ni uongo, kwa sababu mimi nilikuwa Iringa tangu Desemba 24 hadi juzi Januari 4 ndiyo nimerudi Dar es Salaam. Sasa nilikutana lini na hao wazee?”amehoji.
SIMBANAYANGA21
Pamoja na hayo, Poppe amesema madai kwamba hataki Mo anunue hisa nyingi Simba SC kwa sababu itashindikana kulipwa fedha zake alizotumia kusajili nayo ni uzandiki mtupu.

“Mimi siudai hata senti uongozi huu wa Simba SC uliopo madarakani. Fedha ambazo bado ninadai ni wakati wa uongozi wa Rage (Alhaj Ismail Aden) nilitoa fedha za kusajiliwa Emmanuel Okwi (dola za Kimareani 40,000, zaidi ya Sh. Milioni 80) ambazo tulikubaliana nitalipwa akiuzwa Etoile du Sahel,”.

“Nasi sote tunajua kwamba zile fedha hadi leo hazijalipwa. Sina wasiwasi, najua Etoile wakilipa, nami nitapewa haki yangu. Sasa nawatahadharisha watu wanaosema maneno ya uongo, waache, vinginevyo nitawachukulia hatua na wasije kunilaumu,”