Chriss Brown Achunguzwa Kwa Kumdunda Mwanamke

rihanna-600
Polisi katika jiji la Las Vegas, Marekani wanachunguza madai kwamba mwanamuziki mashuhuri wa R&B Chris Brown alimpiga mwanamke Mwishoni mwa wikii.
Mwanamke huyo ambaye jina lake halikuwekwa bayana anadai msanii huyo alimgonga usoni alipojaribu kumpiga picha.
150504175428-chris-brown-april-2015-super-169
Kisa hicho kinadaiwa kutokea katika hoteli alimokuwa Chris Brown mapema Jumamosi asubuhi huku Mwanamuziki huyo hajazungumza lolote kuhusiana na madai hayo.
Mwaka 2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna.