Hiddink Anamatumaini Chelsea Kumaliza Nne Bora

GuusHiddinkITV_960966
Meneja wa Chelsea Guus Hiddink amesema bado inawezekana klabu hiyo kumaliza katika nne bora Ligi ya kuu ya Uingereza baada matokeo mazuri ya timu hiyo waliyoyapata mwishoni mwa wiki dhidi ya Crystal Palace ya 3-0

Klabu hiyo ya Stamford Bridge ilicheza mechi nne bila kushindwa, kwa mara ya kwanza msimu huu, na kupanda hadi nambari 14 mwa ligi.

Hata hivyo, bado wapo nyuma ya Pointi 13 ili kufika eneo la kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Ushindi wao dhidi ya Palace, waliokuwa wanashika namba saba katika ligi, uliibua matumaini kwamba huenda wakafanya vyema kipindi hiki cha pili cha msimu.

Hiddink aliongeza kuwa Kila mmoja anajua kwamba wana wachezaji wazuri lakini wakati mwingine, timu baada ya kutawazwa mabingwa, hulegea.
Moja ya malengo ya Kocha huyo tangu atue Chelsea alisema kuwa ikiwezekana wapate nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya litakuwa jambo nzuri sana japo alikiri kuwa ni vigumu kwa sababu ligi imekuwa na ushindani sana huku Kila timuakisema inaweza kushinda.