Benitez Atimuliwa Real Madrid, Zidane Apewa Kazi

_75820356_zinedine_zidane-getty1
kocha Rafael Benitez ambaye ana Miezi 7 tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu ametimuliwa na Uongozi wa klabu ya Real Madrid kutokana na Matokeo mabovu ya Klabu hiyo na kutokuwa na mahusiano mazuri na wachezaji.

Baada ya kibarua kuota nyasi kwa Benitez Sasa nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mkongwe wa klabu hiyo raia wa mfaransa Zinedine Zidane ambaye awali alikuwa Kocha wa Kikosi B cha Real Madrid.
Real ilitoka Sare 2-2 na Kikosi cha Gary Neville, Mchezaji wa zamani wa Man United ambae sasa anaifundisha Valencia, iliyotoka 2-2 na Real Uwanjani Mestalla katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Atletico Madrid
CX4pjyPU0AEvQhE
Tangu atue Madrid, Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona, pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey

Pia kutupwa nje ya Copa del Rey baada ya kumchezesha Mchezaji asiestahili katika Mechi na Cadiz kumechochea chuki dhidi yake.

Hali hiyo imefanya kuwepo minong’ono ya kila mara kuwa Wachezaji wa Real hawana raha na Benitez na wana mgomo baridi dhidi yake.
Wiki iliyopita Benitez aliwatuhumu Wanahabari kwa kuendesha kampeni kumpinga yeye, Klabu na Rais wao Florentino Peréz.