Timu ya Arsenal wameendelea kutamba katika ligi kuu ya Uingereza na kuweka gepu la Pointi kwa kuwa kileleni mwa hiyo baada ya ushindi dhidi ya Newcastle bao 1-0 lililofungwa na Laurent Koscielny kipindi cha pili, na kufikisha alama 42.
Leicester City wanaowafuata baada ya Arsenal walipoteza nafasi ya kujiimarisha baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Bournemouth, licha ya Bournemouth kucheza mwishoni mwa mechi na wachezaji 10 baada ya Simon Francis kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo mshambuliaji Jamie Vardy.
Uwanjani Old Trafford, ni shangwe kwa meneja Louis van Gaal baada ya vijana wake kuandikisha ushindi wa 2-1, mabao yao mawili wakifungiwa na Anthony Martial na nahodha Wayne Rooney.
Kwingineko, Southampton walilazwa 1-0 ugenini Norwich City, bao hilo likifungwa baada ya kiungo wa kati wa Southampton kutoka Kenya Victor Wanyama kupewa kadi nyekundu.
Uwanjani Stadium of Light, Sunderland wamelaza Aston Villa 3-1.
Katika mechi ya awali, Liverpool walilazwa 2-0 na West Ham.
Matokeo kamili:
• West Ham 2-0 Liverpool
• Arsenal 1 -0 Newcastle
• Leicester 0-0 Bournemouth
• Man Utd 2-1 Swansea
• Norwich 1 -0 Southampton
• Sunderland 3-1 Aston Villa
• Watford 1-2 Manchester City
• West Brom 2-1 Stoke
Ratiba ya Leo Januari 3
C. Palace vs Chelsea – Selhurst -10:30
Everton vs Tottenham – Godson- 10:00