Cheryshev Aiponza Real Madrid Copa del Rey

denis-cheryshev
Real Madrid wamepoteza rufaa yao dhidi ya uamuzi wa shirikisho la soka la Uhispania wa kuwaondoa michuano ya Copa del Rey kwa kumchezesha mchezaji asiyefaa.
Mabingwa hao mara 19 waliadhibiwa kwa kumchezesha winga Denis Cheryshev dhidi ya Cadiz hatua ya 32 bora mnamo 2 Desemba.

Cheryshev alikuwa amefungiwa mchezo mmoja kutokana na kadi za manjano alizoonyeshwa akichezea Villarreal kwa mkopo.

Mahakama ya kutatua mizozo ya kimichezo nchini Uhispania ilitupilia mbali rufaa ya Real baada ya tathmini za taarifa kutoka pande zote.
Klabu hiyo bado inaweza kukata rufaa lakini itahitajika sasa kwenda kwa mahakama za kawaida.