Van Gaal: Sijiuzulu Ng’oo, Tutapambana hadi Mwisho


Kocha wa Manchester United Louis van Gaal, amesema haoni haja ya kujiuzulu baada ya timu yake kutoka sare ya 0-0 na Chelsea uwanjani Old Trafford hapo jana.

Van Gaal alisema wachezaji wanaweza kucheza kwa kiwango kizuri wakiwa kwenye shinikizo hivyo haoni sababu ya kujizulu
Kocha huyo amekua kwenye shinikizo kubwa ya kumtaka kujiuzulu kufuatia kikosi hicho kuchapwa michezo minne mfululizo kipigo cha mwisho kikiwa kutoka kwa Stoke City Jumamosi walipocharazwa 2-0.

Man United wameshindwa kupata ushindi katika michezo minane ya mashindano yote waliyoshiriki msimu huu. Hii ni mara ya kwanza klabu hiyo kufanya hivyo tangu mwaka 1990.

Gaal amesema kwa sasa Wachezaji wamejitolea kupambana nay eye kama Meneja pia amejitolea kupigana, Wakufunzi na bodi pia ina imani kuwa watafanya vizuri