FIFA Bado Yanuka Rushwa, Tokyo Ahojiwa

tokyo-sexwale.png
Mmoja wa wagombea wa kiti cha Urais wa shirikisho la soka duniani FIFA Mosima Gabriel “Tokyo” Sexwale raia wa Afrika Kusini, amehojiwa kuhusiana na madai ya ufisadi wakati wa maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia.

Tokyo Sexwale amefika mbele ya majaji wa Marekani katika jiji la New York, kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusiana na madai ya ulaji rushwa ndani ya FIFA.

Sexwale amefika huko kama shahidi muhimu baada ya shirika la upelelezi la Marekani FBI kumtaka kufika mbele ya majaji mwezi huu.
Alikuwa mojawepo wa wanachama wa halmashauri kuu iliyokuwa inapigia debe Afrika Kusini kupewa uwenyeji wa maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010

Madai ya Marekani kwamba pesa hizo alilipwa Warner kupitia akaunti ya FIFA, na kufichwa kama pesa za kukuza soka, ili kupata kura nyingi zaidi kwa Afrika Kusini kupata zabuni ya uwenyeji wa kuandaa mashindano hayo.
.