Mourinho Avizia Kibarua Cha Van Gaal

2419942_heroa
Tayari tetesi za Kocha aliyetimuliwa katika klabu ya Chelsea Jose Mourinho kuchukua mikoba ya meneja wa sasa wa klabu ya Manchester United Luis Van Gaal zimeanza kusambaa.

Gazeti la The Sun Limeripoti kuwa mara baada ya Manchester United kufungwa Jumamosi na Norwich na pia kuondolewa mapema katika ligi ya Mabingwa Ulaya bado kunaendela kumwekea mazingira magumu kocha wa timu hiyo kuendelea na kibarua chake hapo Old Traford

Mourinho ameeleza kuwa licha ya kufukuzwa kazi wiki iliyopita hataweza kuchukua mapumziko, kwa sasa yupo tayari kufanya kazi na timu yoyote itakayomuhitaji.

“Kwa kweli nina wasiwasi kuhusu pia sikupenda maamuzi ambayo uongozi wa Chelsea wameufanya dhidi ya Mourinhokwa sababu watu wanatakiwa wawe na imani na mameneja wao” Van Gaal aliwaambia waandishi wa habari