Arsenal Kuikabili Man City Leo

455357378
Baada ya kushuhudia michezo mbali mbali ya Ligi kuu nchini Uingereza ikiendelea Mwishoni mwa Wiki, ligi hiyo inatarajia kuendelea tena leo jumatatu pale Arsenal itakapo ikaribisha Man City.

Mchezo huo ndio utatoa sura kamili ya nani atakaye shika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi baada ya Leicester City mwish9oni mwa wiki kuilaza Evertone mabao 3-2 na kuendelea kung’ara kileleni ikiwa na pointi 38.

Mchezo huo utapigwa majira ya 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Emirates unaomilikiwa na Arsenal.
Endapo Arsenal watashinda mchezo huo itaendelea kubaki nafas ya pili kwa kuwa na pointi 36 na kuiacha City nafasi ya tatu kwa pointi 30.