Barcelona Watwaa Ubingwa Kombe la Klabu Bingwa

2747318_big-lnd
Barcelona ndio mabingwa wa dunia wa 2015 wa kombe la klabu bingwa,Mabingwa hao wa Uhispania waliibuka washindi baada ya kuilaza River Plate 0-3 katika fainali iliyofanyika jana nchin Japan.

washambulizi wa Barca Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar wanaifanya timu hiyo kupata Ushindi wa 5 msimu huu.
Messi ndiye alifunga bao la kwanza dakika ya 36” ya mchezo mara baada ya mapumziko Luiz Suarez alitumia vyema pasi nzuri kutoka kwa Sergio Busquets na kufunga bao la pili
2747232_full-lnd
Suarez hakuachia hapo alihakikishisia Barca ushindi alipotikisa wavu kunako dakika ya 68.
Bao hilo la pili lilimpa mshambuliaji huyo machachari wa Uruguay mabao 5 katika mechi mbili baada ya kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa nusu fainali dhidi ya Guangzhou Evergrande.