Messi Kuikosa Fainali Michuano ya Kombe la Vilabu

Lionel+Messi+FC+Barcelona+v+Levante+UD+La+SsbnkA_Mkgsl
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Leonel Messi yupo hati hati kukosa mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la dunia la vilabu inayofanyika Nchini Japan

Messi anasumbuliwa na tumbo huku Klabu ya Barcelona hawajthibitisha kama ataweza kucheza au kutocheza watakapoikabili klabu ya River Plate.

Mshambuliaji Luis Suarez ndiye na Neymar ndio wanategemewa katika safu ya ushambuliaji kwa sasa
Barcelona wameingia fainali baada ya kuifunga Guangzhou Evergrande mabao 3-0 yote yakifungwa na Suarez

Nayo Timu ya River Plate, ilikua timu ya kwanza kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia la vilabu,Baada ya kuibuka kidedea mbele ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya Sanfrecce Hiroshima kwa bao 1-0 .