Manchester United Yapigwa, Chelsea Oyeeee

2427182_heroa
Klabu ya Leicester City imeendelea kujiweka katika mzingira mazuri katika kulitwa ligi kuu ya Uingereza Msimu Huuu baada ya kuisambaratisha Everton mabao 3-2

Nayo Chelsea wamerejelea kwa ushindi baada ya kulaza Sunderland 3-1 mechi yao ya kwanza bila Jose Mourinho aliyefutwa Alhamisi.
Uwanjani Old Trafford, mambo yamemwendea mrama meneja Louis van Gaal baada ya vijana wake wa Manchester Utd kukabidhiwa kichapo cha 2-1 na Norwich City.
Kwingineko uwanjani Goodison Park, Leicester wameendelea kushangaza ulimwengu wa soka kwa kukwamilia kileleni EPL kwa kulaza Everton 3-2.
ross-barkley
Kufuatia kushindwa Jumamosi, Manchester United sasa wamo nambari tano kwenye jedwali wakiwa na alama 29 sawa na Spurs ambao wamo nambari nne lakini wanawazidi kwa magoli.
United wamo alama tisa nyuma ya Leicester walio kileleni wakiwa na alama 38. Nambari mbili na tatu zinashikiliwa na Arsenal ikiwa na pointi 33 na Manchester City pointi 32, klabu zote mbili zikikutana kesho Jumatatu.
Matokeo kamili yalikuwa kama ifuatavyo:
• Chelsea 3-1 Sunderland
• Everton 2-3 Leicester
• Man Utd 1-2 Norwich
• Southampton 0- 2 Tottenham
• Stoke 1-2 Crystal Palace
• West Brom 1 -2 Bournemouth