Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Akabidhiwa Ofisi Rasmi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dk. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akipokea taarifa ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dk. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.

NA Eleuteri Mangi – MAELEZO

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dk. Seif Rashid leo jijini Dar es salaam.

Akipokea ofisi hiyo, Waziri Ummy alimshukuru Dk. Seif kwa jitihada kubwa waliyofanya ya kupambana na magonjwa kwa wananchi na kufanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi duniani ambayo imetatua tatizo la ugonjwa wa polio na kuwa “polio free”.

Aidha, Waziri Ummy amemhakikishia Dk. Seif kuendelea kushirikiana naye pale msaada wake utakapohitajika kwa kuwa anauzoefu katika masuala ya afya ili kuwahudumia Watanzania na kupambana na adui wa taifa ambaye ni magonjwa.

Akikabidhi ofisi, Dk. Seif aliwapongeza Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kupewa nyadhifa hizo na kuahidi kuwapa ushirikiano wake paleutakapohitajika. Dhana ya “Hapa Kazi Tu” imechukua mkondo wake ambapo hadi sasa Mwaziri na Manaibu waziri wanatekeleza dhana hiyo kwa vitendo na siyo kukaa ofisini, kwa kwa juhudi hizo viongozi kwa kushirikiana na wananchi, Tanzania itafanikiwa kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ikiwa na watu wenye afya bora inayowaruhusu kufanyakazi kwa juhudi na maarifa ili kuwa maendeleo yenye tija kwa Wtanzania.