Chelsea Yafumuliwa, Leicester City Yarudi Kileleni

josemourinho-cropped_tb3i5tnk19rl1m3e0v47y9iu1
Klabu ya Leicester City Usiku wa leo imefanikiwa kurudi Kileleni mwa ligi kuu England baada ya kuifunga Chelsea bao 2-1 na kufanikiwa kuipiku Arsenal iliyokua Kileleni kwa kufikifasha pointi 35.

Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy alianza kuifungia timu yake bao la kwanza katika katika ya 34 ya mchezo. Winga Riyard Mahrez akaongeza bao la pili na la ushindi katika dakika ya 48 ya mchezo.

Hata hivyo Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Chelsea lilifungwa na Loic Remy aliyefunga kwa kichwa baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Pedro.

Kwa ushindi huu Leicester City wanarejea kileleni mwa ligi wakiwa na alama 35 baada ya kucheza michezo kumi na sita huku Chelsea wakibaki katika nafasi 16 wakiwa na alama 15 kwa kupoteza michezo tisa katika michezo 16.

Jamei Vardy ameendelea kuongoza katika kinyang’anyiro cha mfungaji bora msimu huu akiwa sasa ametikisa nyavu mara 15 ligi msimu huu.