UEFA: Arsenal Mdomoni mwa Barcelona, Chelsea na PSG

gun__1450090848_141512_Barca
Klabu ya Arsenal ya Uingereza imepangwa na Barcelona ya Uhispania, ambao ndio mabingwa watetezi, kwenye hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mechi hiyo itakuwa kama marudio ya fainali ya 2006, ambayo mabingwa hao wa Uhispania walishinda 2-1 kupitia mabao mawili ya dakika za mwisho mjini Paris.
2318562_w1
Wenzao kutoka Uingereza Chelsea wamepewa miamba wa Ufaransa Paris Saint Germain baada ya droo kufanywa mjini Nyon, Uswisi. Hii itakuwa mara ya tatu mtawalia kwa Chelsea kukutana na PSG katika michuano ya Uefa.
Droo kamili:
• Benfica (Ureno) v Zenit St Petersburg (Urusi)
• Dynamo Kyiv (Ukraine) v Manchester City (Uingereza)
• Juventus (Italia) v Bayern Munich (Ujerumani)
• PSV (Uholanzi) v Atletico Madrid (Uhispania)
• PSG (Ufaransa) v Chelsea (Uingereza)
• Arsenal (Uingereza) v Barcelona (Uhispania)
• Gent(Ubelgiji) v Wolfsburg(Ujerumani)
• Roma (Italia) v Real Madrid (Uhispania)
Mechi za kwanza kucheza Februari 16-17 na 23-24. Mechi za marudiano ni Machi 8-9 na 15-16.