Benki ya Dunia ‘Yalia’ na Mauaji ya Albino Tanzania

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bi. Flora juu ya picha ya mtoto wenye ulemavu wa ngozi.

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bi. Flora juu ya picha ya mtoto wenye ulemavu wa ngozi.

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird kwa uzuni akitafakari baada ya kuitazama picha ya watoto wenye ulemavu wanguzi.

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird kwa uzuni akitafakari baada ya kuitazama picha ya watoto wenye ulemavu wanguzi.

Mkurugenzi wa Makumbusho nchini, Prof Audax Mabula akimshukuru Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia kwa kutembelea Makumbusho kujionea onesho la mateso yanayowapata watu wenye ulemavu wangozi.

Mkurugenzi wa Makumbusho nchini, Prof Audax Mabula akimshukuru Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia kwa kutembelea Makumbusho kujionea onesho la mateso yanayowapata watu wenye ulemavu wangozi.

Na Sixmund J. Begashe

WATANZANIA wamehusiwa kuwapenda watu wenye ulemavu wa ngozi kama albino, na kuachana kabisa na imani putofu kuwa viungo vya watu hao vinaweza kuwapatia bahati katika maisha yao, kama inavyoaminika kwa baadhi ya watu waovu hapa nchini.

Wito huu umetolewa na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia hapa nchini, Bella Bird alipotembelea Makumbusho ya Taifa kujionea onesho maalum la picha zinazoelezea namna watu wenye ulemavu wangozi wanavyo nyanyasika kwa kuishi maisha ya wasiwasi kuofia waovu wenye nia mbaya na miili yao.

“Onesho hili linaumiza sana rohoo, linaumiza tena sana, maana linanifanya na mimi nihisi kama ndio mmoja wa hawa watoto wanaoishi katika kambi hii ya Kabanga, hawawezi kutoka nje na kufurahi na watoto wenzao, hawawezi kuishi na wazazi wao, hii inaumiza sana” alisema Mh Bird huku akitokwa na Machozi.

Mh Bird ameendelea kwa kutoa wito kwa vyombo vya habari kusaidiana na Makumbusho ya Taifa katika kuielimisha jamii kwa kupitia njia hii adhimu na yakisayansi ili jamii ielimike na kuondokana na fikra potofu za kuwauwa na kuwakata viungo watu wenye ulemavu wa ngozi.

Akimshukuru Mkurugenzi huyo Mkazi wa Benki ya Dunia hapa Nchini kwa ofisi yake kudhamini onesho hilo, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabula ameahidi kuwa Makumbusho ya Taifa itaendeleza kampeni za utokomezaji wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kutoa elimu kwa jamii ili waachane kabisa na tabia hiyo ya ukatili.

Prof. Mabula pia alitumia nafasi hiyo kumwomba, Bird ofisi yake ifikirie namna ya kuiwezesha Makumbusho ya Taifa kulitembeza onisho hilo hasa sehemu kuu zilizo adhirika na Mauaji ya watu wenye ulemavu wangozi kama Mikoa ya Mwanza na Shinyanga ambapo Mkurugenzi huyo alikubaliana na ombi hilo na kuwa atalifanyia kazi.

Prof. Mbula aliendelea kwa kuziomba taaisisi mbali mbali, za serikali na zile za binafsi kuisaida Makumbusho ya Taifa kuendeleza vita hii ya mauaji ya kinyama hapa nchini ili kuwafanya watanzania wote waishi kwa amani kwani sisi sote kama watanzania ni sawa na kila mmoja atambue kuwa kila mtu anahaki ya kuishi.

Onesho hilo la picha lenye kuonesha namna gani watu wenye ulemavu wa ngozi albino wanavyoishi kwa shida, mashaka, uzuni, hofu, hawako huru kama watu wengine, limefanyiliwa na Benki ya Dunia na litaendelea kuoneshwa hadi mwishoni mwa mwezi wa Kwanza hapo mwakani.