Droo ya EUFA Kufanyika Leo Uswisi.

140828174348_sorteio_uefa_champions_league_getty_624x351_getty
Hatma ya vilabu vya Uingereza katika Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya Itajulikana leo mara baada ya kufanyika kwa Droo hiyo mjini Uswisi.

Mechi za raundi ya mtoano ya timu 16 bora zinazoshiriki klabu bingwa ulaya itajulikana kama Arsenal wataendelea kubaki kwenye midomo ya wakali wa soka Duniani Barcelona kama inavyozungumzwa na wengi au laa.

Katika droo hiyo kuna makundi mawili na cha kwanza ni lile la Washindi wa Makundi ambao watapangwa na Mpinzani kutoka kundi la Pili la Timu zilizoshika Nafasi ya Pili kwenye Makundi yao.

Lakini kwa mujibu wa kanuni za Uefa Klabu kutoka Nchi moja na zile zilizokuwa Kundi moja haziwezi kupambanishwa.

Wakati huo huo Uefa itapanga ratiba ya michuano ya Europa ligi, michuano hiyo inashirikisha timu 32 huku timu 8 zikiwa ni zile ziliondolewa katika michuano ya klabu bingwa kwa kushika nafasi ya tau kila kundi.