TP Mazembe Watolewa Michuano ya Vilabu Dunia.

501182396
wawakilishi wa Afrika katika michuano ya kombe la Dunia la Vilabu iliyoanza Disemba 10 nchini Japani,Klabu ya PT Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imechapwa na wenyeji wa michuano hiyo timu ya Sanfrecce Hiroshima mabao 3-0.

Wenyeji Hiroshima walipata mabao yao kupitia Tsukasa Shiotani, Dakika ya 44, Kazuhiko Chiba, 56, na Takuma Asano, akifunga bao la mwisho.
2744282_xbig-lnd
TP Mazembe ambayo inachezewa na watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kushiriki michuano hiyo.

kipigo hicho kinainyima nafasi timu ya Tp Mazembe kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hivyo watachuana na Klabu America, ya Mexico, ambayo nayo ilichapwa kwa mabao 2-1 Guangzhou Evergrande.
Kwenye nusu fainali Sanfrecce Hiroshima, watawachuana na River Plate, huku Barcelona wakikipiga na Guangzhou Evergrande.