Waziri Ummy Mwalimu Siku ya Kwanza Ofisini

IMG_8317

Gari la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu likiwasili Makao Makuu ya wizara hiyo na kupokelewa kwa saluti mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika sherehe zilizofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

IMG_8321

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando mara tu baada ya kumalizika kwa tukio la kuapishwa.

IMG_8324

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando (kulia) kuelekea ofisini kwake.

IMG_8325

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.

IMG_8329

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni ofisini kwake huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando akishuhudia tukio hilo.

IMG_8346

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala akiwasili katika wizara ya hiyo moja kwa moja akitokea Ikulu baada ya kula kiapo.

IMG_8347

Pichani juu na chini ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.

IMG_8350

IMG_8354

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkaribisha Naibu wake Dk. Hamis Kigwangala ofisini kwake.

IMG_8356

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala ofisini kwa Ummy Mwalimu.

IMG_8359

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Ummy Mwalimu.

IMG_8374

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu wake Dk. Hamis Kigwangala. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Gideon Malabeja. Chanzo Mo Blog.