Hatari: Homa ya Nguruwe Yaibuka Mwanza

Homa ya Nguruwe Yaibuka MwanzaKUMETOKEA mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe (African Swine Fever) Wilaya ya Nyamagana, Kata za Mabatini, Mirongo kishiri na Buhongwa na Igoma. Mlipuko huu umedhibitishwa kwa uchunguzi uliofanyawa na Maabara ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA). Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe unasababishwa na Virusi (African Swine fever virus).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Dk. Yohana D. Sagenge kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, imesema ugonjwa umeibuka katika Wilaya ya Nyamagana, Kata za Mabatini, Mirongo kishiri na Buhongwa na Igoma. Taarifa imeeleza kuwa madhara ya ugonjwa huo ni makubwa kwa wafugaji na kiuchumi kwani husababisha vifo asilimia 100 kwa Nguruwe wote walioambukizwa.

Imesema kuwa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe hauna chanjo wala tiba na hauambukizi Binadamu. Njia pekee ya kudhibiti ugonjwa huu ni kuzuia kuenea kwa maambuzi toka eneo lenye maambukizi kwenda eneo lisiloambukizwa.

Aidha taarifa hiyo imewataka wafugaji kufuanya yafuatayo kukabiliana na ugonjwa huo;  Wafugaji waepuke kununua Nguruwe kutoka kwenye Maeneo/Mashamba yenye ugonjwa,  Nguruwe wafugwe kwenye Mabanda imara na waepuke kutembea ovyo,  Nguruwe wasilishwe mizoga au masalio ya chakula kutoka vyanzo visivyojulikana
,  Teketeza Mizoga iliyokufa kwa ugonjwa na ufanye usafi kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam na kwa kutumia dawa za kuua vimelea vya magonjwa (disinfectants).

Mengine ni pamoja na  Wakulima watoe taarifa ya uwepo wa ugojwa haraka kwa mtalaa wa Mifugo aliye karibu,  Wananchi wazingatie maelekzo yote yanaotolewa pindi watalaam wa Mifugo wanapoweka Tangazo la Karantini (QUARANTINE) la kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe.