Mchezaji Olivier Giroud raia wa Ufaransa jana alifungia Arsenal mabao matatu kwa mara yake ya kwanza na kuihakikishia The Gunners kusonga mbele katika ligi ya Mabingwa Ulaya na kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuwafunga Olympiakos mabao 3-0.
Arsenal walihitaji kushinda kwa mabao 2-0, au 3 -1 ili kusonga mbele katika kundi F.
Giroud alianza kwa kufunga kwa kichwa kipindi cha kwanza, kisha akafunga la pili dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza kwa pasi safi kutoka kwa Joel Campbell.
Mfaransa huyo aliihakikishia Arsenal wanafuzu kwa kufunga la tatu kupitia mkwaju wa penalty.
Arsenal hawajawahi kukosa kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu kuanza kwa mfumo wa sasa 2003-4, na walionyesha uzofu wa kusakata gozi katika jukwaa kuu Ulaya kwa kung’aa katika uwanja wa Athens.
Matokeo kamili ya mechi za UEFA zilizochezwa Jumatano:
• Bayer Leverkusen 1 – 1 Barcelona
• Olympiakos 0 – 3 Arsenal
• Chelsea 2 – 0 FC Porto
• Valencia 0 – 2 Lyon
• Roma 0 – 0 BATE Borisov
• Dinamo Zagreb 0 – 2 Bayern Munich
• Dynamo Kiev 1 – 0 M’bi Tel-Aviv
• KAA Gent 2 – 1 Zenit St Petersburg
Kwa matokeo hayo sasa Timu za Real Madrid, Wolfsburg, Atletico Madrid, Man City, Barcelona, Bayern Munich, Chelsea na Zenit ndio timu ambazo zimeongoza katika makundi na kuungana na timu nyingine katika hatua ya 16 bora, na kuingia droo ya raundi ya muondoano ya timu 16 ambayo inatarajiwa kufanyika Desemba 14.