Lil Kim Kuachia Albam Baada ya Mwaka Mpya.

lil-kim-32755
Lil Kim amewambiwa mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani yupo njiani kwa kuachia burudani kali mwanzoni mwa januari mwaka ujao.

Kim Hajatoa Albam kwa kipindi cha miaka 10 licha ya kuwa na nyimbo nyingi, na sasa anasema atakuja kivingine ili kuwalidhisha mafansi wake waliokuwa wakimsubili kwa ujio wake mpya.
lilkimandsnoop

Baada ya kufurahia kuwa mama kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, Kim ameamua kurudi kufanya kazi ambapo imebainika kwamba amekuwa akitumia muda mwingi studio kufanya mambo.

“Ninafanya kazi kwa juhudi na albamu mpya inakaribia kutoka kwa mwanzoni mwa mwaka ujao,” alisema Kim na kuongeza kuwa yeye anajua mengi yameongelewa juu ya ukimya wake.
gfgffgfggggggggg
Kim amesema katika kila nafasi atafanya vizuri kutokana na sababu nyingi kwanza yeye anataka kuweka upendo kwa mashabiki, na sasa watu wanafuraha na kuwa na tabasamu kusikia yupo njiani kuachia ngoma kali baada ya ukimya wa muda mrefu.