MWANASOKA DAVID BECKHAM AGEUKIA RUGBY.

beckham-cropped_925qqeumw2va182b5vzxjie5nMchezaji wa Zamani wa Uingereza na Nahodha wa Manchester United David Beckham amebainisha yeye anafurahia kutazama mchezo wa raga zaidi ya soka kwa sababu ya mazingira ya kifamilia katika michezo.

Beckham, ambaye aliichezea Klabu Manchester United na Real Madrid na kumfanya kushida mataji mbali mbali na kuiletea sifa kubwa taifa la Uingereza.

Akizungumza na Radio Times, Bekham alisema: “I love raga – napenda kuangalia na ni mpenzi zaidi wa mchezo huo kuliko soka kwa sasa.

“Naurahia kwenda kwenye viwanja vya mchezo huo mara nyingi na Nimefurahia kuangalia mpira wa namna hiyo japo sina klabu maalumu ninyoshabikia”

Beckham alisema alitumia muda mwingi kwenda kuangalia mechi za mpira soka alipokuwa mtoto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, alisema imani yake kwamba nchi yake mwaka 2018 na 2022 katika kombe la Dunia wanapaswa kufanya vizuri zaidi.

Alisema licha ya kasfa za rushwa zinaoendelea kuikabili FIFA haina budi mashindano hayo kufanyika Urusi na Qatar kama ilivyopangwa kuliko kuanza kuangalia upya nani aandae

“Kama ni rushwa au la,tayari nchi hizo zimechaguliwa. Watu wanahitaji kusonga mbele sio kuangalia nyuma walikotoka” Beckham aliongeza.