DNA: naipenda sana Familia Yangu.

dna10
Kukutana DNA mzee wa Banjuka Raia wa nchi ya Kenya akitanua na familia ya katika nchi za mambele.

mwanamuziki DNA aliyetamba na Kibao cha Banjuka anasema anaonafuraha zaidi anapokuwa akitanua akiwa na familia yake kuliko anapokuwa mwenyewe.

Wimbo wa Banjuka wakati ukitoka mwaka 2007 ulikuwa kama wimbo wa taifa hasa kwa vijana kutokana na kupendwa kwa wimbo huu uliomtoa kisanii DNA.

Hata hivyo baada ya kutoweka katika sekta ya muziki kwa muda mrefu,DNA amedai alikuwa bize zaidi kuihudumia familia yake kitu ambacho kilionekana kama vile anapotea kwenye game la mziki.

Licha ya kutoa nyimbo kadhaa lakini DNA amedai kuwa familia yake inafuraha zaidi kuusikia wimbo wa Banjuka ukigogwa kwenye vyombo vya habari.

Msanii huyo Pia amekuwa akichukua likizo kwenda nje ya nchi akimaanisha kuwa maisha yake bado ni mazuri, tofauti na watu wanavyozungumza kuwa kipato chake kimeshuka.