Timu kutoka Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu imefanikiwa kutwaa ubingwa katika michuano ya SHIMMUTA ilimalizika mwanzoni mwa wiki hii jijini Hapa.
Timu hiyo imefanikiwa kutangazwa kuwa mabingwa baada ya kunyakua vikombe vingi katika michuano hiyo iliyokuwa inajumuisha zaidi ya michezo 12 na zaidi ya Timu 20 zilijitokeza katika michuno hiyo iliyofanyika kwa siku tano tangu Setemba 26 hadi septemba 30 mwaka huu.
Michezo ilikuwa inashindaniwa ni pamoja na riadha, kuvuta kamba, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Miguu, Drafti, kukimbia na gunia, Bao,na mchezo wa vishale.
Timu shiriki ni pamoja na vyuo mbali mbali ikiwemo SUA, UDOM, UDSM, MUHASI, ATC,IAA, MUCCobs, Ardhi, na Mzumbe, pia taasisi na makamuni mbalimbali yalikuwepo yakishiriki ni pamoja na TANESKO, TANAPA, TBS,NEMC, Mipango, TPDC, AICC, na AUWASA.
Mgeni rasmi katika ufungaji wa michuano hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkuru ambapo alisisitiza na kuwasihi wanamichezo kudumisha fani zao hata wanapokuwa sehemu zao za kazi.
“Michezo huleta watu pamoja kwa umoja, ushirikiano, na umoja mfano mzuri mnaona hapa watu wametoka Mbeya, Mwanza na wengine Dar es Salaam, lakini wote tumekuwa kitu kimoja”Alisema Nkuru
Aidha Katibu mkuu wa SHIMMUTA Award Safari alisema kuwa licha ya kupokea malalamiko kutoka sehemu mbalimbali juu ya mashindano hayo hasa katika timu ya shirika kuchezesha mamruki watalifanyia kazi katika mashindano yajayo.
“Pia Uongozi wa SHIMMUTA umesikitishwa na uongozi chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kwa kuitoa timu isiendelee kushiriki katika ya michuano hii kwani imeleta usumbufu kutokana na kuwa ilikuwa tayari imeanza mashindano “aliongeza safari.