Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA), Kipo katika hali ya ukata mkubwa kiasi ambacho kilisababisa kushindwa kwenda kushiriki Michuano ya Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba Mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA) Barick Kilimba alisema kuwa licha ya chama kuandaa kikosi kwa ajili ya mashindano, walishindwa kufanikisha lengo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuelekea Dodoma yalikokukuwa yanafanyika mashindano hayo.
“Tulikuwa tusafirishe watu kumi na mbili wakiwemo viongozi wawili na wachezaji kumi , lakini kiasi ambacho tulikuwa tumekipata hakitoshi kuwasafirisha watu hao kwakuwa bajeti yetu ilikuwa Milion 3 na nusu lakini tulifanikiwa kupata milioni 2 pekee.”
“Tulitoa taarifa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa nao wakapeleka taarifa kwa Afisa wa Michezo wa Mkoa ambaye alitusaidia kutupa kibari cha kusambaza barua kwenye Mkampuni mbalimbali na sio kutupatia fedha,ambapo tulifanikiwa kusambaza barua zaidi ya Ishirini lakini hatukufanikiwa” alisema Kilimba.
ARBA walithibitisha kushiriki mashindano ya kitaifa hivyo itawapasa kulipa ada ya shilingi laki moja ikiwa kama adhabu ili kuwawezesha kupata mwaliko mwingine hapo mwakani.
Kikosi kinachounda timu ya Kikapu ya Mkoa wa Arusha ni Phabian Mjarifu, Cristian Joseph, Elly Bombo, Seta Magabe, Bery Rubbert, Robert Edward, Benny Mkangala, Deo Minja, Baraka Lowasa, Faisal Khan na Rymond Yusuph.
Wengine wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Sune Mushendwa, Timmoth Ngalula, Bariki Kilima, James Kinruwah, na Kelvin Hozza.
Kikosi hicho kinanolewa na Walimu watatu ambao ni Ahmed Hamad, William Kidje na Aloyce Aloyce.
“Hata hivyo chama Cha Kikapu cha Taifa, kilitakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kusaidia baadhi ya huduma sio kila kitu vyama vya Mikoa vifanye wakati wao ndio wapo juu, ajabu wameviachia vyama vya Mikoa vifanye vyenyewe kitu ambacho ni Mzigo Mkubwa” alisema Kilimba.