MONREAL AKIRI KUSHINDWA KUZUNGUMZA KINGEREZA

monreal1Beki wa kushoto wa Timu ya Arsenal Nacho Monreal amesema kuwa anajisikia vizuri zaidi na amani anapokuwa katika uwanja wa Klabu hiyo Emerates Stadium.

Monreal ambaye ni raia wa nchi ya Uhispania alijiunga na washika Bunduki hao Januari 2013 akitokea Klabu ya Malaga ya Hispania, na sasa ameonekana kupata namba ya kudumu ndani ya kikosi Cha Mzee Wenger baada ya kupata majeraha ya mara kwa mara kwa Kieran Gibbs.

Beki huyo akizungumiza na mtandao wa timu hiyo “the Arsenal Weekly podcast” aliongeza kuwa Klabu hiyo kwake ni sawa na nyumbani kutokana na mapenzi yake yaliyokuwa hata kabla hajatua kwa washika mtutu hao.

“kila kitu kinakwenda sawa siwezi ona kama niko mbali na nyumbani bali naona niko nyumbani, maana nikisema sijisikii vizuri nadhani ningekuwa nimeshaondoka, napenda kuishi Uingereza, nalipenda jiji la London na Naipenda timu yangu nadhani hapa ni sawa na 100% za maisha yangu”

“Kipindi nafika hapa nilijua jambo la kwanza ninalo takiwa kulifanya ni kujifunza Lugha ya Kingereza, wachezaji wengi na hata wafanyakazi wanazungumza lugha ya Kingereza hivyo ilinipasa nijifunze kwa Bidii, iliniwia vigumu sana kwa sababu ilikua lugha ngumu kwangu hivyo sikuwa na namna ya kufanya Hayo na hadi sasa najitahidi kuogea Kingereza” alisema Beki huyo.

“Mikel, Santi and Hector walikuwa wanafuraha nilipojiunga nao , nilikua siwezi kuongea Kingereza, nilikua sijui kitu chochote wenzangu wanachokiongea ila akina Ateta ni Wahispania wenzangu walinisaidia Kutafsili kwa kuwa wao walijifunza mapema hii lugha.”