WATANZANIA wametakiwa kuwapelewa watoto wao katika vyuo mbalimbali vya ufundi stadi elimu inayo zalisha ajira nyingi kuliko vyuo vikuu hapa nchini ili kuepukana na tatizo la ajira.
Inadaiwa kuwa watu wanaojiajiri ni wengi wanao toka katika vyuo vya ufundi kuliko wanano maliza vyuo vikuu kutokana na wanao toka vyuo vikuu wanategenea kuajiliwa huku wa vyuo vya ufundi wakijikita kujitengenezea ajira na kuachana na utegemezi kutoka kwa wazazi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya vyuo vya Veta kamda ya nyanda za juu inayo jumuisha mikoa ya Iringa, Ruvuma na Njombe, Kabaka Ndenda, juzi katika mahafari ya kwanza kwenye chuo pekee ya wilaya cha Veta Makete, alisema kuwa vijana wengi wanao maliza katika vyuo vya ufundi wanauhakika wa kujiajiri kuliko wanao enda vyuo vikuu.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakiona ni bora kumpeleka mtoto wake katika chuo kikuu kuliko kumpeleka katika vyuo vya ufundi, alisema kuwa Tanzania kutokana na ulivyo mfumo wa ajira watoto ni bora wakapelekwa katika vyuo vya ufundi ili kutengeneza ajira.
“Tanzania tulikataa mfumo wa mwalimu Nyerere wa ujamaa tukataka ukabaila wakati hatuwezi kwenda nao ndio maana tunapata shida kupata ajira, Tanzania bado hatujafika hatua ya kusoma vyuo vikuu na kupata ajira moja kwa moja,” alisems Ndenda.
Alisema kuwa licha ya vijana hao wanao fuzu mafunzo kuweza kujiajiri wanatakiwa kuhakikisha kuwa wakitoka hapo wanaenda kuunda vikundi ili waweze kukopesheka.
Hata hivyo wanafunzi hao waliiomba serikali kuhakikisha kuwa inawapa sapoti pale watakapo kuwa wameunda vikundi vyao na kuweza kujikwamua kimaisha kwa kupata mikopo kutoka serikalini.
Mkuu wa chuo hicho Ramadhani Sebo alisema kuwa wanafunzi hao wanaenda kuajirika licha ya kuwa na changamoto za vifaa vya kufundishia katika baadhi ya fani zinazo fundishwa katika vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na katika fani ya ufundi magari.
Alisema kuwa wanafunzi katika chuo hicho wamefanya mafunzo kwa vitendo na wameiva vyakutosha kwenda kuingia katika kujiajiri katika ufundi na kuanza kujitegemea.
Alisema kuwa chuo hicho kwa sasa ambacho ni chapekee cha wilaya Tanzania nzima na kuwa kilianza na kozi mbili na sasa kina kozi 4 huku kikifundisha masomo mtamboka.
Alisema kuwa kutokana na kuto kuwa na mabweni chuo hicho wanafunzi wake wamepanga mitaani na kuwa baadhi ya wanafunzi wameshindwa kumaliza chuo kutokan ana changamoto za kutoka mbali na