Bunge Lamthibitisha Waziri Mkuu Majaliwa, Apata Kura 258

Rais John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi, Kassim Majaliwa jimboni kwake enzi za kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

Rais John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi, Kassim Majaliwa jimboni kwake enzi za kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.


BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitishwa Mbunge wa Ruangwa(CCM), Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Kassim Majaliwa amethibitishwa na Bunge baada ya kupigiwa kura na kupata jumla ya kura 258 za ndio ikiwa ni sawa na asilimia 73.5 ya kura zote. Ni kura 91 tu ikiwa ni sawa na asilimia 25.5 ndiyo zilizomkataa kiongozi huyo mteule na kiranja wa mawaziri wajao. Jumla ya kura halali 351 zilipigwa katika zoezi hilo huku kura mbili zikiharibika.

Akizungumza na wabunge kutoa shukrani Kassim Majaliwa alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuongoza Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kisha kumteuwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Waziri Mkuu huyo mteule anatarajiwa kuapishwa kesho Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma zoezi litakaloanza saa nne kamili asubuhi.