Akitangaza matokeo hayo mchana huu, Katibu wa Bunge, Dk. Joseph Kashililah alisema Ndugai ameshinda baada ya kupata kura 254 kati ya kura 359 zilizopigwa na wabunge wote walioshiriki uchaguzi huo katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Ndugai amemshinda mpinzani wake mkubwa kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Godluck Ole Medeye aliyepata jumla ya kura 109. Wagombea wengine wote hawakuambulia kura yoyote katika kinyang’anyiro hicho. Ndugai ambaye katika Bunge la 10 alikuwa na nafasi ya Naibu Spika alizaliwa Januari 21, mwaka 1960.