Dk. Mengi Agharamia Ukarabati Ngazi Kuu za Hospitali ya KCMC

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya ngazi kuu za kuingilia wodini katika hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya ngazi kuu za kuingilia wodini katika hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Dk. Geleard Masenga wakati alipowasili katika ofisi ya Mkurugenzi  huyo mwishoni mwa wiki. 
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisalimiana na Askofu mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria (KKKT) Tanzania, Dk. Fredrick Shoo alipowasili katika ofisi ya Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya KCMC. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hopstali hiyo, Dk. Gileard Masenga.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akiteta jambo na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria (KKKT) Tanzania, Dk. Fredrick Shoo .
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akipeana mikono na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Dk. Gileard Masenga mara baada ya kutamburishwa kuwa ndiye mtendaji mkuu wa hospitali hiyo kwa sasa.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza jambo mara baada ya utamburisho wa mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Dk. Gileard Masenga akizungumza jambo mbele ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani).
Dk. Mengi akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mkurugenzi mkuu wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC, Dk. Giliard Masenga akizungumza kuhusu ujenzi wa ngazi kuu za kungilia wodini katika hosptali ya Rufaa ya KCMC ambazo ujenzi wake uligharimu kiasi cha milioni 30, Fedha ambazo zilitolewa na Dk. Mengi.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria, (KKKT) Dk. Freedrick Shoo akisoma taarifa ya Hospitali hiyo katika hafla fupi ya uzinduzi wa ngazi kuu za kuingilia wodini katika hospitali ya rufaa ya KCMC, ujenzi uliofadhiliwa na Dk. Mengi.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria, (KKKT) Dk. Freedrick Shoo akimkabidhi Dk. Mengi taarifa ya Hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ngazi kuu za kuingilia wodini katika hosptali ya rufaa ya KCMC, ujenzi uliofadhiliwa na Dk. Mengi.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya ngazi kuu za kuingilia wodini katika hospitali hiyo.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo.
Mwenyekiti mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akiongozana na Mkurugenzi mtendaji wa Hopstali ya Rufaa ya KCMC wakipita katika ngazi kuu zilizofanyiwa ukarabati hii karibuni.
Dk. Mengi akitizama baadhi ya maeneo katika wodi za hospitali ya rufaa ya KCMC ambayo miundombinu ya maji pamona na vyoo imekuwa chakavu.
Sehemu ya maeneo ambayo yameathirika na uchakau wa miundo mbinu ya maji.
Dk. Mengi akisalimiana na mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Mkurugenzi mtendaji wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC, Dk. Giliard Masenga akimuonesha Dk. Mengi  maeneo mbali ya hospitali hiyo ambayo upanuzi umeanza kufanyika kama sehemu ya kuboresha huduma ya afya.
Dk. Mengi akiaga mara baada ya kutembelea hospitali ya rufaa ya KCMC pamoja na kuzindua ngazi kuu za kuingilia wodini. Picha na Dixon Busagaga.