Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wakiswali swala ya Idd. Waislamu wote leo wameungana na Waislamu ulimwenguni kote kusherehekea Siku Kuu ya Idd baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. (Picha kwa hisani ya FullShangwe Blog).
Baadhi ya Wanafunzi wa Madrassa ya Tishabab iliyopo Magomeni wakipita mitaa kadhaa ya eneo hilo wakisherehekea Siku Kuu ya Idd.
Wanafunzi wa Madrassa Tishabab ya Magomeni wakisherehekea Idd kwa nyimbo za shukrani kwa Mwenyezi Mungu leo.
Sherehe za Idd zilivyo anza Mitaa ya Magomeni leo asubuhi jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Mpigapicha wa dev.kisakuzi.com)