Katika gazeti la Mzalendo lilikuwa na kichwa cha habari “Wengi Dar watumia maji yenye kinyesi” na upande wa gazeti la Majira lilibeba kichwa cha habari “Maji machafu yaathiri Dar”. Ndani ya habari hizo waandishi wameelezea shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kama moja ya chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu kwa kuwa maji hayo yameathirika na kinyesi.
Gazeti la Majira 08/11/2015 ukurasa wa 3 inanukuliwa “Kwa kiasi kikubwa Maji ya jiji yamekuwa yameathirika na kinyesi cha binadamu”. mwisho wa kunukuu. Aidha nukuu nyingine kwenye gazeti la Majira inasomeka “Wananchi wa jiji la Dar es salaam wamekuwa wakipata Majisafi na salama kutoka mamlaka ya Majisafi na salama (DAWASCO) kwa aslimia 30 tu”.
Ikumbukwe pia maeneo makubwa ambayo wagonjwa wa kipindupindu wanatoka ni maeneo ambayo yameathirika na wizi wa maji kwa kiasi kikubwa na mapambano hayo bado yanaendelea kuhakikisha wizi wa maji unakwisha maeneo hayo ni pamoja na Manzese, Buguruni ,Kigogo , Mburahati , Kinondoni mkwajuni pamoja na Tandale.
Jitihada zilizofanywa na Dawasco katika kudhibiti ugonjwa huu hususa ni watumiaji Maji ni pamoja na Kupeleka huduma ya maji BURE kwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mlipuko huo kupitia utarartibu wa Manispaa uliowekwa, Kutoa Elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari machapisho, pamoja na vikao vya pamoja na watendaji wa Mitaa, Bwana Afya kwa maeneo yaliyoadhirika, kuanza kwa usajili rasmi wa magari yanayofanya biashara ya maji (water bowsers) ili kulinda afya ya mtumiaji. Zoezi lilianza tarehe 01 October 2015 na idadi ya Magari 120 yameshasajiliwa hadi sasa.
Na kuondoa maunganisho yasiyo halali ambayo yanafanywa na baadhi ya wananchi “vishoka” , ambayo yanapeleka huduma ya Maji kwa baadhi ya maeneo yanayoadhirika zaidi. Dawasco inasikitika kwa taarifa hizo za upotoshaji kwani tangu kuibuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu jitahada mbali mbali zimefanyika kwa kushirikiana na Mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Afya , Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ,kikosi cha kupambana na ugonjwa wa kipindupindu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa na taaisi nyingine nyingi zenye kutetea ustawi wa Afya ya Jamii.
Dawasco inapenda kuwakumbusha vyombo vya habari kuzingatia weledi na utashi katika kuteleza majukumu yao ya kila siku ili kuwapatia wananchi taarifa zilizo sahihi na zenye ukweli siku zote. Tunaamini kosa la namna hiyo halitajirudia tena ili kuepusha adha na usumbufu kwa wananchi kama ulivyojitokeza kipindi hiki.