CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Omary Abdallah Kigoda ambaye ni mtoto wa marehemu Dk. Abdallah Kigoda kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Handeni Mjini. Omary Abdallah Kigoda amepata fursa hiyo badala ya kupita katika mchujo wa kura za maoni mara mbili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 4 kwa vyombo vya habari na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Moses Nnauye imeeleza Kigoda ameteuliwa kugombea nafasi hiyo ya ubunge baada ya kushinda kura za maoni za marudio zilizofanyika Novemba 03, 2015.