CCM Yaanza Mchakato Kumsaka Mrithi wa Dk Kigoda Handeni

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipozungumza nao.

Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipozungumza nao.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mchakato wa kumtafuta mwanaCCM ambaye atasimama kwa tiketi ya chama kugombea Jimbo la Handeni ambalo lilikuwa likigombewa na marehemu Dk. Abdullah Kigoda aliyefariki dunia hivi karibuni.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema tayari CCM Handeni imefanya uchaguzi wa awali wa kura za maoni kwa kuwashindanisha wagombea 11 ambao walijitokeza kuomba nafasi hiyo, na nafasi ya kwanza imeshikwa na Omari Abdalah Kigoda ambaye ni mtoto wa marehemu Dk. Abdalah Kigoda huku nafasi ya pili ikishikwa na Hamis Hamad Mnoundwa.

Hata hivyo kamati kuu CCM imeamuru ufanyike mchujo mwingine wa kura za maoni kwa kushindanishwa wagombea wawili waliokaribiana kwa kura ili kuona nani anaweza kukubalika zaidi kwa wanachama wa CCM Handeni kabla ya uamuzi wa mwisho.