LICHA ya baadhi ya ripoti na taarifa za kiuchumi kutoka nchi za Tanzania, Uganda na Kenya kuonesha kuwa uchumi wa nchi hizo umekuwa ukipanda kila uchao, bado baadhi ya familia zinaishi katika makazi duni kupindukia kiasi cha kuhatarisha maisha ya familia hizo.
Nchini Uganda miongoni mwa maeneo ya makazi duni na yenye msongamano kimakazi ni eneo la Katanga ambapo wakazi wake wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
Kenya makazi hayo yapo katika Jiji la Nairobi eneo la Kibera ambalo historia yake ilianza miaka ya 1963, baada ya uhuru wa nchi hiyo. Sensa ya mwaka 2009 inaeleza makazi hayo maarufu duniani yalikadiriwa kuwa na Wakenya 170,070.
Hata hivyo sasa Kibera inakadiriwa kuwa na kati ya wakazi 235,000 hadi 270000. Kwa Tanzania eneo maarufu kimakazi ya aina hiyo ni Manzese lililopo jijini Dar es Salaam. Manzese ambayo ni kata ya Wilaya ya Kinondoni katika jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo kwa mujibu wa sensa iliyofanyika 2002, kata yenye makazi duni na holela ambao wengi wapo katika hatari kiafya hasa ilikuwa na wakazi wapatao 66,866.
Zifuatazo ni picha mbalimbali kuonesha sehemu ya makazi hayo na hatari yake kwa wakazi husika.
Baadhi ya makazi duni ya eneo la Kibera Jijini Nairobi, nchini Kenya.
Baadhi ya picha juu zikionesha makazi duni eneo la Katanga nchini Uganda.
Baadhi ya picha zikionesha makazi duni ya Manzese Dar es Salaam.