Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe enzi za Uhai wake.
Msaidizi wa Mbunge huyo, Casablanga Haule enzi za Uhai wake.
Padri Plasdus Ngabuma enzi za Uhai wake.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika nyumbani kwake Kijichi Dar es Salaam mchana.
Mjane wa Deo Filikunjombe, Sarah (katikati) akisaidiwa na jamaa zake wakati wa ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Padri Maxmillian Wambura kutoka Parokia ya Mtakatifu Wote Kiluvya akiyamwagia mafuta ya baraka majeneza hayo.
Waombolezaji wakiwa katika ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la Plasdus Haule.
Jamilia ya Filikunjombe ikiwa katika ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Nyumba ya Filikunjombe ambayo inadaiwa amekaa wiki mbili tangu ahamie baada ya kukamilika ujenzi wake ‘Hakika tumuache mungu aitwe mungu”
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.PICHA NA MICHUZI JR.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Dk John Pombe Magufuli akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha Mumwe Deo Filikunjombe, wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Dk Magufuli akifarijiana na Zitto Kabwe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Dk Magufuli alishindwa kujizuia kutoa machozi ya huzuni wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele ya waombolezaji wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi mkoani Njombe.