Akizungumza na wakazi wa jimbo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa kampeni zake, Rajabu alisema katika kuboresha afya za wananchi hao atahakikisha anaboresha hospitali zilizopo katika jimbo hilo kutolewa huduma zake zinazofanana na hospitali ya Temeke.
“Ninafahamu mazingira ya watu wa mbagala hivyo nahitaji kutatua kero zenu za barabara, kwa kutanua barabara za mitaa ikiwa ni kuondoa foleni kupungua kwa aslimia 80,”alisema.
Alisema kutokana na kutanua barabara hizo pia atajenga kituo kikubwa cha kisasa cha sanjari na kila kata kuwa na kituo cha afya na kuongeza kuwa kutokana na wananchi wa jimbo hilo kuwa wengi hali ambayo haina uwiano na huduma muhimu kama masoko ataboresha na kuwa la kisasa.
“Soko la Zakhem serikali inasema ni mali yao huku wafanyabiashara wa sokoni hapo wanalipa kodi ya sh.30,000, nikipata nafasi ya ubunge soko hilo litakuwa mali ya umma,”alisema.