kwani kuna baadhi ya watu hasa vijana hawafanyi kazi wakiamka asubuhi kitu wanachokifanya ni kucheza pool huku wakisubiri mabadiliko. “Hata katika vitabu vya dini imeandikwa asiyefanya kazi na asile kwani kazi ni msingi wa maendeleo, hata ukipiga kelele kiasi gani kama hufanyi kazi huwezi kupata mabadiliko katika maisha yako.” “Ndugu zangu Mwenyezi Mungu ametupa akili ya kutambua mema na mabaya tusikubali kudanganywa, mabadiliko ya siku hizi siyo mazuri yanaleta uvunjifu wa Amani kwani watu wamepandikizwa maneno ya chuki wanafanya vurumai na kuharibu vya kwao, wanawachukia ndugu zao imefikia hatua watu hawazikani, hawasalimiani. Lakini hao aliowapandikiza chuki kwao kuna maendeleo,” alisisitiza. Mama Kikwete alisema yeye kama MNEC anadhamana kubwa ya kuhakikisha anakisemea na kukipigania chama chake na kuwataka wananchi hao kushikamana na kuwa kitu kimoja kwa kufanya hivyo wataitunza Amani ya nchi na kuzidi kudumisha upendo katika jamii yao. Aidha aliwasihi wananchi hao kutokubali kurubuniwa na kitu chochote bali wazitunze kadi zao za kupigia kura na siku ya uchaguzi ikifika wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi na kuwachagua viongozi kutoka CCM ambao watawaletea maendeleo ya kweli. Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Nachingwea Hassan Massala aliahidi kama atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo atasimamia ilani ya uchaguzi ya CCM na kuhakikisha huduma za elimu zinaboreshwa hii ni pamoja na shule kuwa na vitabu na walimu wa kutosha na kujenga nyumba za walimu ili watoto wapate elimu bora. Ataboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na dawa zinapatikana kwa wakati. Massala alisema, “Katika jimbo hili, maeneo ya mjini kuna maji ya kutosha lakini kijiji cha Ngunichile kuna tatizo ingawa vyanzo vya maji vipo. Nitahakikisha maji yanapatikana. Kuhusu umeme Serikali inampango wa kusambaza katika vijiji vyote, nguzo zimeanza kusambazwa kinachohitajika ni kusimamia ili zoezi hili liende haraka.” Mgombea huyo wa nafasi ya Ubunge alimuomba Mama Kikwete awasaidie ili mnara wa mawasiliano ya simu uweze kujengwa katika kata ya Ngunichile kwani eneo hilo linashida ya mawasiliano. “Ukiwa katika kijiji hiki huwezi kuwasiliana na mtu yeyote kwa njia ya simu kwa kuwa hakuna mnara wa mawasiliano. Hivi sasa simu ni pesa na simu ni Benki tunaomba Mama yetu utusaidie ili mnara wa mawasiliano ujengwe katika kijiji hiki,” Massala aliomba. Kuhusu ombi la kujengewa mnara wa mawasiliano ya simu katika kijiji hicho ambacho ni kata ya Ngunichile Mama Kikwete aliahidi kulifanyia kazi na kulifikisha kunakohusika. Naye mgombea ubunge wa jimbo la Liwale Faith Mitambo aliwaomba wananchi wamchague ili aendelee kuwatumikia kwa kipindi kingine cha miaka mitano na kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana katika jimbo hilo. Mitambo alisema, “Ilani ya uchaguzi ya CCM inasema itaendelea kuboresha huduma ya afya na ndani ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi Zahanati ya kijiji cha Mbaya itakuwa kituo cha Afya. Aidha Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kuhakikisha umeme unapatikana vijijini kati ya vijiji hivyo kimojawapo ni kijiji hiki. “Nawaomba kura zenu ili mtuchague viongozi kutoka CCM ambao ni madiwani, mbunge na rais ili tuweze kusimamia na kutekeleza kwa vitendo na kuhakikisha yale yote yaliyoandikwa katika ilani ya uchaguzi yanatekelezwa.”
Mabadiliko ya Kweli Yataletwa na Wananchi Wenyewe – Mama Salma Kikwete
http://doxycyclinehyclate-dosage.com/augmentin useshttp://lisinopril-hctz-dosage.com/doxycycline brand nameslisinopril 20 mgsildenafil patentfurosemide inhalationhttp://viagrageneric-price.com/augmentin usesgabapentinsildenafilis cialis better than viagra