Wanawake Wajasiliamali Wanasemanini Juu ya Serikali Iliopo na Ijayo?

RAIA wa Tanzania wenye sifa wanatarajia kupiga kura Oktoba 25 katika Uchaguzi Mkuu kuchagua viongozi ambao wataunda Serikali ya awamu ya tano na kuliongoza taifa kwa kipindi cha miaka 5 mfululizo. Yafuatayo ni maoni ya baadhi ya wanawake wajasiliamali walioshiriki Maonesho ya 39 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam juu ya Serikali inayomaliza muda wake inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete na ijayo.

Bi. Zaydat Selemani

Bi. Zaydat Selemani

Mwanamama mjasiliamali, Bi. Zaydat Selemani kutoka Chukwani Zanzibar anasema;

“…Serikali inayomaliza muda wake imetusaidia kiasi japo si sana ki vile…hasa katika suala la kutukutanisha hapa Sabasaba kwa ajili ya kuonesha bidhaa zetu, lakini pamoja na hayo bado tunachangamoto za masoko ya ndani kwa wajasiliamali akinamama. Kwa upande Serikali ituwezeshe zaidi upande wa uzalishaji na kututafutia masoko ya kudumu ya bidhaa zetu…” anasema Selemani.

Fatuma Hamran Abdullah

Fatuma Hamran Abdullah


Fatuma Hamran Abdullah, Chumbuni, Zanzibar
“…Binafsi nasikitika sana kwa Mheshimiwa Rais wa Tanzania kwani alitoa fedha kwa wajasiliamali zitusaidie kwa upande wa vifunganishi, lakini hizo fedha hazijatufikia hadi leo sisi wajasiliamali kwenye banda la Zanzibar na rais ndio amaliza muda wake je, tutazipata lini? Lakini wametfanzia mema tunapo pa kushika tunaonesha bidhaa zetu hapa.

“…Kwa Serikali ijayo kitu ambacho tunaomba tunaomba tuboreshewe zaidi wajasiliamali maanda ndiyo tunaoiendesha nchi ukienda nchi kama China wajasiliamali ndio wanaoendesha nchi hivyo Serikali itusaidie kwani tunaweza leta mchango zaidi kwenye mapato.

Pia tunaomba Wajasiliamali tunapoingia Tanzania Bara bandarini Dar es Salaam tusinyanyaswe maana sisi ni Watanzania hilo waelewe na bidhaa zetu zipitiswe kwa uhakika sio kupekuliwa kama tunavusha bangi…siye atuvushi bangi tunahakika na bidhaa zetu sote tunaipenda Serikali yetu hatuwezi kufanya jambo baya kwani vita ikitokea wanaoteseka ni sisi wanawake hivyo tunaomba tusinyanyaswe bandarini,” anasema Bi. Abdullah.

Bi. Luce Josephat Urio

Bi. Luce Josephat Urio

Bi. Luce Josephat Urio kutoka Chukwani Zanzibar

“…Serikali iliyopita kwa kweli imetusaidia kutufanya tuelewe haki zetu na kutumia fursa zilizopo kujuendeleza kijasiliamali hadi hatua tuliyonayo sasa. Kwa Serikali ijayo inatakiwa ijue mazuri tuliofanyiwa na Serikali iliyopita nayo ifanye mazuri zaidi, itufanye tujitegemee na kuwa na makampuni makubwa ili tuweze kuitangaza nchi yetu…itusaidie vitu kama vifungashio vya bidhaa na namna ya kuziandaa kiubora na kuzitangaza zaidi,” anasema Bi. Hamran Abdullah.

Bi. Khadija Juma Mohammed

Bi. Khadija Juma Mohammed

Bi. Khadija Juma Mohammed natoka Kisiwa cha Pemba, Zanzibar

“…Serikali nashukuru imetuwezesha wajasiliamali na kutupatia sehemu kama hizi za kuja kwenye maonesho kujitangaza na pia kupata changamoto na kujifunza zaidi, tunashukuru sasa tumepiga hatua. Kwa serikali inayokuja tunaomba ituinue zaidi akinamama ili tuweze kufanya vizuri zaidi tupande maendeleo…akinamama pia nawashauri wawe wajasiliamali wachakarike na kuacha kuwa tegemezi nyumbani maana watazidi kukandamizwa,” alisema Bi. Juma Mohammed.

Maoni haya yametolewa na baadhi ya Wanawake wajasiliamali walioshiriki Maonesho ya 39 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mwisho